VIDEO: Muuza mitumba aondoka na gari la Diamond Platnumz

Muktasari:

Tukio hilo limetokea Agosti 14,2018 katika Ofisi za Wasafi zilizopo Mbezi Beach,ambapo Diamond amesema shindano hilo limefanyika mwezi mmoja kupitia bidhaa za Diamond.

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye pia Mkurugenzi wa WCB,amemkabidhi gari mshindi wa Shindano la Nogewa Ushinde aitwaye Bakari Saidi.

Tukio hilo limetokea Agosti 14,2018 katika Ofisi za Wasafi zilizopo Mbezi Beach,ambapo Diamond amesema shindano hilo limefanyika mwezi mmoja kupitia bidhaa za Diamond.

Diamond amesema,lengo la kufanya shindano hilo ni  kuwajali mashabiki zake, kutokana na kumpa sapoti katika hatua zote hadi alipofikia hapa.

"Nawaheshimu sana mashabiki zangu,na naimani aliyeshinda ni mmjo wa mashabiki zangu,hivyo shindano hili la Nogewa Ushinde,ni moja ya kuwapa zawadi kutokana na hatua zote nilizopitia hadi kufika hapa," alisema Diamond.

Kwa upande wa Bakari ambaye ni muuza mitumba Ubungo alisema, anashukuru kwa zawadi hiyo kwani hakutegemea kama atakabidhiwa zawadi yake kutokana na kushinda muda mrefu huku akiwa anasubiri zawadi.

"Namshukuru sana Diamond kwa kunikabidhi gari hii,ambayo nilikuwa nalisubiria kwa muda mrefu, nilipata kuponi yangu iliyoandikwa hongera umeshinda gari, nikaileta kuwaonyesha wakaniambia nisubiri watanipigia simu. Mimi sikutaka kuiacha kuponi yangu nikawa nasubiria kuitwa.

" Ndio hadi jana nilipopigiwa simu kuwa nakuja kukabidhiwa gari yangu leo, "alisema Bakari.