Mv Kazi rasmi kazini

Muktasari:

  • Hayo yamesemwa leo, Jumatatu  na Waziri mwenye dhamana hiyo Profesa Makame Mbarawa wakati akipokea kwa niaba ya serikali kivuko kipya kinachofahamika kama MV Kazi.
  • Kivuko hicho kitakachofanya safari kati ya Feri na Kigamboni ujenzi wake umegharimu Sh7.3 trilioni na kina uwezo wa kubeba watu 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.

Dar es Salaam. Wizara ya Ujenzi, Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi imeahidi kuendelea kutafuta njia mbalimbali kukabiliana na changamoto ya usafiri hasa katika maeneo yanayotegemea vivuko.

Hayo yamesemwa leo, Jumatatu  na Waziri mwenye dhamana hiyo Profesa Makame Mbarawa wakati akipokea kwa niaba ya serikali kivuko kipya kinachofahamika kama MV Kazi.

Kivuko hicho kitakachofanya safari kati ya Feri na Kigamboni ujenzi wake umegharimu Sh7.3 trilioni na kina uwezo wa kubeba watu 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.

Profesa Mbarawa amesema kivuko hicho kinakwenda kusaidia changamoto ya usafiri kwa wakazi wa Kigamboni ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia ufanisi mbovu wa vivuko vilivyopo.