Mvua kubwa kunyesha Dar

Muktasari:

  • Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wananchi waishio mabondeni kuchukua tahadhari kufuatia mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha siku mbili mfululizo kuanzia kesho Septemba 26,2018
  • Mikoa inayotarajia kukumbwa na mvua hizo ni Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar


Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadharisha kutokea mvua kubwa ndani ya siku tatu kuanzia kesho hadi Alhamisi Septemba 27, 2018,.

Kutokana na utabiri huo, TMA imewataka wananchi kuchukua tahadhari.

Taarifa ya mamlaka hiyo, iliyotolewa leo jioni Septemba 25,2018 imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni Tanga, Dar es Salaam, Pwani pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.

Taarifa hiyo imewataka wananchi wa maeneo husika kuchukua tahadhari kwa sababu mvua hizo ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 70.

“Madhara yatakayotokana na mvua hiyo ni kutokea mafuriko katika mitaa na kusababisha msongamano wa magari na watu hivyo kuchelewesha usafirishaji hasa katika maeneo ya mjini,” imesema taarifa hiyo ya TMA