Mwaka 2016 haukuboresha maisha ya wananchi- Zitto

Zitto Kabwe

Muktasari:

Akizindua kampeni za chama hicho katika Kata ya Kijichi, Dar es Salaam, Zitto alisema Serikali inapaswa kuendelea mapambano dhidi ya ufisadi lakini pia kuimarisha hali za wananchi.

Dar es Salaam. Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema mwaka 2016 ulikuwa wa utumbuaji na majipu na kusahau kuongoza na kuboresha maisha ya wananchi.

Akizindua kampeni za chama hicho katika Kata ya Kijichi, Dar es Salaam, Zitto alisema Serikali inapaswa kuendelea mapambano dhidi ya ufisadi lakini pia kuimarisha hali za wananchi.

Akimnadi mgombea wa chama hicho, Edgar Mkosamali, mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema,“Sisi kama chama hatuna tatizo na mapambano ya Serikali dhidi ya ufisadi na rushwa, lakini ni vyema mapambano hayo yakaenda sambamba na kuimarisha hali za watu na hilo ndilo tatizo la walio wengi.”