Mwakyembe Mgeni Rasmi Tuzo Ligi Kuu

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuongoza hafla ya utoaji tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau wa mpira wa miguu kutoka kada tofauti wakiwemo viongozi wa soka, wachezaji, viongozi wa serikali, makocha, wadhamini pamoja na wachezaji wa zamani.

Tayari Waziri Mwakyembe ameshaingia ndani ya ukumbi huu mnamo saa 2.15 usiku na amepokelewa na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kabla ya Waziri Mwakyembe kuingia, washindani wa tuzo za vipengele tofauti walitangulia wakiwa wamevaa suti ambazo zimeandaliwa na kamati inayoratibu na kusimamia tuzo za Ligi Kuuu