Mwananchi yatoa wateule 13 tuzo za Ejat

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga

Muktasari:

Waandishi walioingia kwenye hatua hiyo ya mwisho ni Kelvin Matandiko, Florence Majani, Janeth Mesomapya, Deogratius Kamagi, Jackline Masinde, Sauli Giliad na Alawi Masare.

Dar es Salaam. Kampuni ya Mwananchi Communications imendelea kung'ara kwenye tuzo za umahiri zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kufanikiwa kuingiza fainali jumla ya kazi 13 kati ya 36 zinazowaniwa kwenye upande wa magazeti.

Waandishi walioingia kwenye hatua hiyo ya mwisho ni Kelvin Matandiko, Florence Majani, Janeth Mesomapya, Deogratius Kamagi, Jackline Masinde, Sauli Giliad na Alawi Masare.

Wengine ni Hellen Nachilongo, Nuzulack Dausen, Dionis Nyato,Peter Nyanje, Majuto Omary na Musa Juma.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Kajubi Mukajanga alisema mwandishi wa habari mkongwe Jenerali Ulimwengu ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya utoaji wa tuzo hizo. 

Alisema jumla ya kazi 810 ziliwasilishwa na kati ya hizo 66 ndizo zilizofanikiwa kuingia hatua ya fainali.

Kati ya hizo 36 za magazeti,16 radio na 14 za runinga.