Mwanafunzi adai alijifunza kulawitiwa toka kwa wazazi wake

Muktasari:

Hoja yao imetokana na taarifa kuwa baadhi ya watoto wa kiume katika Shule ya Msingi Kaloleni wamelawitiwa na wa kike kufanya mapenzi na watu wazima.

Moshi. Wananchi mbalimbali wa mjini hapa mkoani Kilimanjaro, wakiwamo wasomi na viongozi wa dini, wametaka uchunguzi wa watoto wadogo kudhalilishwa kingono ufanyike katika shule zote za msingi.

Hoja yao imetokana na taarifa kuwa baadhi ya watoto wa kiume katika Shule ya Msingi Kaloleni wamelawitiwa na wa kike kufanya mapenzi na watu wazima.

Hata hivyo, baada ya Gazeti la Mwananchi kufanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi, mmoja alikiri kufanyiwa kitendo hicho na mwanafunzi mwenzake kwenye makalavati ya barabarani.

Alipoulizwa alijifunzia wapi mchezo huo alisema, “nilikuwa nawaona baba na mama wanafanya ndiyo nikaamua nijaribu. Lakini toka tupelekwe polisi nimeacha kabisa huo mchezo.”

Taarifa za shule hiyo ambazo zimethibitishwa na viongozi wa Serikali, zimekuja miezi minane tangu vitendo vya aina hiyo vibainike katika Shule ya Msingi Msaranga katika Manispaa ya Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema suala hilo liligunduliwa na walimu wakati wakiwahoji wanafunzi ambao maendeleo yao kitaaluma yalionekana kushuka.

Soma habari kamili katika Gazeti la Mwananchi