Mwanafunzi wa kitanzania ashinda insha Umoja wa Mataifa
Muktasari:
Naburi ni Mtanzania anayesoma Chuo Kikuu cha African Leadership, huko Mauritius na walitakiwa kuandika kwa lugha sita zinazotumika na Umoja wa Mataifa. Lugha hizo ni Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi
Mwanafunzi wa Kitanzania, Amani Alfred Naburi, ni mmoja wa kati ya wanafunzi 60 kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali duniani ambao wameshinda shindano la Insha lijulikanayo kama “Lugha nyingi, Dunia Moja” ( Many languages, One World) lililoandaliwa kwa ushirikiano baina ya United Nations Academic Impact ( UNAI) na ELS Educational Services, Inc.
Naburi ni Mtanzania anayesoma Chuo Kikuu cha African Leadership, huko Mauritius na walitakiwa kuandika kwa lugha sita zinazotumika na Umoja wa Mataifa. Lugha hizo ni Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi
Washindani wa Insha hiyo walitakiwa kuandisha Insha juu ya namna watakavyochangia katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( Agenda (2030). Ambapo kila moja wapo alitakiwa kuiandika insha hiyo yenye maneno yasiyozidi 2,000 kwa lugha nje ya lugha yake ya asili ya nchi anayotoka.