Mwandishi wa gazeti la Habari Leo afariki dunia

Muktasari:

Simba (46) pia alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC). Katibu wa chama hicho, Bryson Mshana alisema jana kuwa Simba alilazwa hospitalini hapo akitokea Hospitali ya Ligula mkoani Mtwara akisumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo kwa takriban miezi miwili.

 Mwandishi wa habari wa kujitegemea wa gazeti la Habari Leo mkoani Mtwara, Hassan Simba (pichani) amefariki dunia jana katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Simba (46) pia alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC). Katibu wa chama hicho, Bryson Mshana alisema jana kuwa Simba alilazwa hospitalini hapo akitokea Hospitali ya Ligula mkoani Mtwara akisumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo kwa takriban miezi miwili. Mtoto wa marehemu, Ally Simba alisema baba yake alifariki dunia saa 7:20 mchana na mazishi yatafanyika leo Kijiji cha Tingi wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Simba alipata Shahada ya Mawasiliano kwa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Washington, akisoma kwa njia ya masafa na Stashahada ya Uandishi wa Habari kutoka Nyegezi Social Training Institute mwaka 1995.

Kabla ya kuandikia Habari Leo kuanzia mwaka 2007, aliandikia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. (Mwandishi Wetu)