Mwanzilishi wa Facebook apewa shahada ya heshima Chuo Kikuu cha Havard

Marekani. Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckeberg amepewa shahada ya heshima ya sheria na Chuo Kikuu cha Havard jana.

Zuckerbag ambaye ni mtu wa tano kwa tajiri duniani,aliacha masomo kabla ya kuhitimu katika Chuo hicho cha Havard na kujikita zaidi akibuni mtandao huo maarufu duniani.

Katika hotuba yake Zuckerberg amewaambia wahitimu kwamba;

 "Tunaishi katika wakati ambao haujaimarika".

"Hizi ndizo jitihada za wakati wetu, nguvu za uhuru, uwazi na jamii ambayo itaondoa utawala wa kimabavu na kuzuia utengano,” amesema

Kabla ya kutoa hotuba hiyo, alipokea shahada ya staha ya sheria.

Zaidi ya watu bilioni 1.9 huingia Facebook kila siku.

Tangu kuzinduliwa kwake mnamo 2004, Facebook imezusha ushindani katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, Snapchat na Instagram.