Wednesday, January 11, 2017

Mwenyekiti Karagwe ajionea uharibu chanzo cha maji

By Juhudi Felix, Mwananchi jfelix@mwananchi.co.tz

Karagwe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Wallesi Mashanda amesema chanzo cha maji cha Kabagendera kumeharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu.

Kutokana na hali hiyo, amewaagiza watendaji wa umma katika maeneo yote ya vyanzo vya maji kuvilinda kwa ajili ya maisha ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Amesema atakayeshindwa kutunza mazingira awe tayari kutumia mshahara wake kupanda miti hiyo.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ihembe, amesema suala la kulinda vyanzo vya maji halina itikadi za kisiasa kwa sababu linalohusu maisha na masilahi ya jamii bila kujali tofauti zao.

Mkazi wa eneo hilo, Irene Kitale amewaomba wagombea wa vyama vyote kutekeleza ahadi zao za uchaguzi.

Mhandisi wa Maji Wilaya ya Karagwe, Walter Kirita amesema licha ya Serikali kujitahidi kutekeleza miradi ya maji katika Kata ya Ihembe, bado upatikanaji umekumbwa na changamoto ya kijiografia inayosababisha kutopatikana kirahisi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wananchi kutoka vijiji vitatu vya Iteja, Mwamnga na Lubuga uliofanyika eneo la Viwanja vya Shule ya Msingi Iteja, pia amewataka viongozi wa Serikali za mitaa kuacha kutumia rasilimali za umma kujinufaisha.“Badala ya kutumika kwa masilahi ya jamii inayohifadhi msitu wa kijiji, hifadhi imekuwa ikiwanufaisha viongozi ambao huwatoza faini wanaoingiza mifugo hifadhini na kujilipa posho. Tabia hii lazima ikome mara moja,” ameagiza Sweda.

Hifadhi hiyo imekuwa ikitunzwa na kijiji husika kama eneo maalumu la utunzaji miti na maliasili zingine za misitu na imekuwa kivutio cha watalii wa ndani.

-->