Mwenyekiti wa mtaa ashikiliwa na polisi kuhamasisha vurugu mtaani

Wananchi wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa wamekaa juu ya mawe barabarani wakimtaka mkandarasi anayejenga barabara hiyo zaidi ya mwaka mmoja kumwaga maji ili kupunguza vumbi. Picha na Stella Ibengwe

Muktasari:

  • Wananchi walidaiwa kufunga barabara wakidai kwamba wanaathirika na vumbi

Shinyanga. Wananchi wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga wameifunga kwa mawe barabara inayoendelea kujengwa na kampuni ya ukandarasi  ya Jasco Investment, kwa madai ya kuchoshwa na vumbi.

Pia Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde na mwenyekiti wa mtaa huo Diana Ezekiel wakishikiliwa na jeshi la polisi.

Wananchi hao walifanya tukio hilo jana saa tano asubuhi katika eneo hilo huku wakiongozwa na mwenyekiti wa mtaa huo, wakidai kuchoshwa na  vumbi kali linatokana na mchanga na saruji baada ya magari kupita eneo hilo. 

Wakati Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari akishikiliwa kwa muda wa saa mbili na kuachiwa kwa madai ya kupiga picha tukio hilo, mwenyekiti wa mtaa anashikiliwa kwa madai ya kuhamasisha wananchi kufunga barabara.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule alisema walikamatwa watu wawili akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo na mwanamume mmoja akipiga picha.

“Huyo mwananume mwingine alipofikishwa kituoni akahojiwa alijitambulisha kama mwandishi wa habari hivyo akaachiwa bila masharti lakini mwenyekiti wa mtaa huyo bado tunamshikilia,” alisema Kamanda