Mwigulu azindua bodi mpya ya Parole -VIDEO

Nchemba ataka utaratibu mpya kushikilia mahabusu

Muktasari:

  • Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye bwalo la maofisa wa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam leo, Mwigulu amesema nyenzo ya msingi ya utekelezaji huo ijikite kwenye mambo matatu ikiwamo kuelewa vizuri mpango wenyewe, uelewa wa sheria na ya mpango huo na taratibu zake za utekelezaji na uelewa wa utaratibu mzima wa ufuatiliaji wafungwa watakaonufaika na utekelezaji wa mpango huo.

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezindua bodi mpya ya taifa ya Parole baada ya ile ya awali kumaliza muda wake wa miaka mitatu.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye bwalo la maofisa wa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam leo, Mwigulu amesema nyenzo ya msingi ya utekelezaji huo ijikite kwenye mambo matatu ikiwamo kuelewa vizuri mpango wenyewe, uelewa wa sheria na ya mpango huo na taratibu zake za utekelezaji na uelewa wa utaratibu mzima wa ufuatiliaji wafungwa watakaonufaika na utekelezaji wa mpango huo.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Augustino Mrema alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni elimu ndogo miongoni mwa watu ambapo wamekuwa wakisema anaingilia kazi za wengine.