Mwijage ajitoa kimasomaso kutetea hoja ya viwanda

Muktasari:

“Unaweza kuwa ni fundi upo kijijini, una cherehani nne na unafahamika na uongozi wa kijiji ukapewa kazi ya kushona nguo kwa ajili ya wanafunzi wa tarafa nzima ikiwa na watoto zaidi 2,000 ukishona hizo sare zao wote, nakuapia mwakani cherehani 26... sasa kwa nini tusikiite kiwanda?” alihoji.

Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amefafanua kauli yake aliyoitoa bungeni dhidi ya wajasiriamali wadogo wanaotakiwa kuanza kulipia kodi. Alitoa ufafanuzi huo zikiwa zimepita siku chache tangu alipotaka wenye cherehani kuanzia nne kuhesabiwa kama kiwanda na waingizwe katika mfumo wa kulipia kodi jambo ambalo lilizua gumzo katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Unaweza kuwa ni fundi upo kijijini, una cherehani nne na unafahamika na uongozi wa kijiji ukapewa kazi ya kushona nguo kwa ajili ya wanafunzi wa tarafa nzima ikiwa na watoto zaidi 2,000 ukishona hizo sare zao wote, nakuapia mwakani cherehani 26... sasa kwa nini tusikiite kiwanda?” alihoji.

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa duka la vifaa vya ujenzi linalomilikiwa na raia wa China, Mwijage alisema mtu akiwa na vyerehani kuanzia nne hadi vinane anaweza kufanya mambo makubwa.

Alisema Watanzania hawapaswi kudharau cherehani, kwa sababu asilimia kubwa ya nguo zinashonwa kwenye mashine hizo.

Mwijage alisema wananchi wanapaswa kubadilika na kuwa wazalendo kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, badala ya kuzipa kipaumbele bidhaa za nje.

“Hawa wenzetu (Wachina) hawakimbilii kutafuta vifaa vya ujenzi kutoka nje, bali wanatambua wawekezaji wa Tanzania, wanafanya kazi na wataalamu wa hapa na kuwaelekeza jinsi ya kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa,” alisema.

Naye Balozi wa China nchini, Lv Younqing alisema ripoti ya Umoja wa Kimataifa inaonyesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya tisa kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji.

“Kupitia fursa hiyo Tanzania itakuwa daraja muhimu sana kiuchumi, kwa nchi nyingine zinazoizunguka,” alisema Younqing.

moja, kwa kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji ambayo ndiyo yatatumika viwandani.

“Viwanda vingi nchini vinatarajiwa kuwa vile vinavyotegemea mazao za kilimo, jambo ambalo litaongeza faida kwa wakulima na ajira, kwa kuwa bado Tanzania haijafikia uwezo wa kuwa na viwanda vikubwa vya kutengeneza magari,” alisema.

Alisema ili dhana ya Tanzania ya viwanda ifanikiwe vyema, ni kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora na Serikali inatenga nchi katika kanda za kilimo cha mazao ya mbalimbali.