Sunday, January 21, 2018

Mwijage alia kutonunuliwa bidhaa zinazozalishwa nchini

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage 

By Mussa Juma,Mwananchi mjuma@mwananchi.co.tz

Arusha. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kuunga mkono agizo la Rais John Magufuli la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kununua bidhaa zinazozalishwa nchini.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 21, mwaka 2018, Mwijage amesema manunuzi ya vifaa kutoka nje kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya taasisi za Serikali, kuacha kununua vinavyotengenezwa nchi ni kwenda kinyume na agizo la Rais.

"Lazima hizi taasisi kuonyesha uzalendo wao kwa kununua bidhaa za ndani zenye ubora, kwanza watawezesha viwanda kufanya kazi lakini pia wataongeza pato la taifa na ajira kwa watanzania,” amesema Mwijage.

Amesema Serikali inafuatilia michakato ya zabuni mbalimbali, kuona kama inakwenda sambamba na maagizo ya Serikali, kwamba  uzalendo wa watendaji wa taasisi hizo pia utapimwa kwa kutekeleza maagizo ya serikali.

"Hili ni suala ambalo lazima tushirikiane ni zaidi ya uzalendo kwani kama kuna bidhaa zenye viwango zinazalishwa nchini, kwanini taasisi yako  katika miradi yake ikanunuwe vifaa nje,"amehoji.

 

 

-->