Mwijage azindua kituo cha manunuzi ya vifaa vya ujenzi

Dar es Salam. Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amefungua kituo cha manunuzi ya vifaa vya ujenzi (Building Centre) kinachomilikiwa na raia wa China.

 

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa duka hilo Mwijage amesema uwepo wa maduka ya aina hiyo utawasaidia watu kurahisisha mfumo wa manunuzi.

 

 "Ile dhana ya kutoka duka moja kwenda duka jingine na kupata vitu tofauti na kuibiwa kwa sasa umekwisha na badala yake unakuja humu ndani unanunua lila kitu unamaliza." Amesema