Friday, April 21, 2017

Mwili wa Ely Macha wawasili viwanja vya bunge

Mwili wa mbunge Dk Elly Macha ukiwasili katika

Mwili wa mbunge Dk Elly Macha ukiwasili katika viwanja cha Bunge mjini Dodoma 

By Reginald Miruko, Mwananchi rmiruko@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwili wa mbunge, Dk Elly Macha aliyefariki dunia Uingereza umewasili katika viwanja vya Bunge leo Ijumaa tayari kuagwa na wabunge wenzake.

Spika wa Bunge, Job Ndugai na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa waliupokea mwili huo na baadaye kutolewa salamu za makundi mbalimbali.

Akisoma wasifu wa marehemu,  mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ameeleza historia ndefu ya kutafuta elimu hadi udaktari wa falsafa akiwa mlemavu wa kuona.

Mchungaji Msigwa amesema watu wenye ulemavu hufahamika kwa kufanya mambo ya kawaida lakini wale wasio na ulemavu hujulikana kwa kufanya mambo yasiyo ya kawaida.

Dk Macha alifariki dunia Machi 31, 2017 katika hospitali ya New Cross nchini Uingereza kwa ugonjwa wa kupungukiwa damu.

 

-->