NMB yazindua huduma mpya ya NMB Wakala

Mkuu wa Idara ya Njia Mbadala wa Benki ya NMB, George Kivaria

Muktasari:

  • Huduma hiyo itawawezesha wateja kufanya miamala na kulipia huduma mbalimbali ambazo hapo awali zilimlazimu mteja kupanga foleni kwenye tawi.
  • Akizindua huduma hiyo leo Mkuu wa Idara ya Njia Mbadala, George Kivaria amesema imelenga kuwafikia kwa ukaribu zaidi wateja wake ambao wapo katika maeneo mbalimbali nchini.

Dar es Salaam. Benki ya NMB imezindua huduma ya NMB Wakala itakayowawezesha wateja wake kupata huduma za benki hiyo wakiwa katika mazingira yao.

Huduma hiyo itawawezesha wateja kufanya miamala na kulipia huduma mbalimbali ambazo hapo awali zilimlazimu mteja kupanga foleni kwenye tawi.

Akizindua huduma hiyo leo Mkuu wa Idara ya Njia Mbadala, George Kivaria amesema imelenga kuwafikia kwa ukaribu zaidi wateja wake ambao wapo katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema kupitia mawakala zaidi ya 2000 wateja wa NMB watapata huduma mbalimbali ikiwemo malipo ya luku, maji, kodi, muda wa maongezi, ving’amuzi, mihamala ya kutuma fedha na ada za shule.