Naibu Waziri ataka vijiji 8,000 vipate umeme

Muktasari:

Mtunguja amesema mpaka sasa vijiji vingi havijapata umeme licha ya Sh4.5 bilioni kutumia na kwamba Tanesco wanatakiwa kuongeza kasi ya kusambaza umeme huo vijijini ili kufanikisha malengo ya Serikali.

Mbeya. Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Merdad  Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania  (Tanesco) mkoani hapa kuhakikisha vijiji 8,000 vya mkoa huu vinapata umeme kupitia kabla ya 2025. Dk Kalemani ametoa agizo hilo leo (Alhamisi) mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa  miradi  mbalimbaliiliyotolewa na Katibu Tawala Mkoa, Mariam Mtunguja kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliyotembelea mkoani hapa.

Mtunguja amesema mpaka sasa vijiji vingi havijapata umeme licha ya Sh4.5 bilioni kutumia na kwamba Tanesco wanatakiwa kuongeza kasi ya kusambaza umeme huo vijijini ili kufanikisha malengo ya Serikali.

Kutokana na taarifa hiyo, Kalemani amewataka  viongozi wa mkoa kufuatilia na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo tayari Serikali ilishatoa fedha ili kwenda  na kasi ya Rais John Magufuli .