VIDEO: Nape: Siondoki CCM nina hisa

Muktasari:

Ametoa kauli hiyo jana Jumapili Julai 15, 2018 wakati akizungumza  na wananchi wa Mtama mkoani Lindi

Mtama. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema hawezi kukihama chama hicho tawala kwa kuwa ana hisa nyingi.

Katibu huyo wa zamani wa Itikadi na Uenezi wa CCM ametoa kauli hiyo jana jioni Jumapili Julai 15, 2018 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mtama katika mkutano wa hadhara.

Amewataka wananchi hao kuondoa hofu juu yake akiwataka kupuuza maneno yanayosema kuhusu hatima yake CCM, kusisitiza kuwa hataondoka katika chama hicho.

“Nimechaguliwa kuwatumikia wananchi wa Mtama. Yapo maneno mengi yanazungumzwa, hasa kuhusu hatima ya mbunge wenu. Tusipate  shida  kwenye   chama  changu  cha  kijani,” amesema Nape.

“Nina hisa nyingi najua mmenielewa, furaha yangu ni kuwatumikia hayo mengine ni bla bla tu.”

Kuhusu asilimia 65 ya ushuru wa zao la korosho kwenda Serikali Kuu, Nape amesema ataendelea kufuatilia jambo hilo na kusisitiza kuwa kuteleza si kuanguka.