Nasa wazuiwa kuanzisha Mabaraza ya Wananchi

Muktasari:

Jaji Lilian Mutende alitoa amri ya muda Jumatatu hadi ilitakapokamilika kusikilizwa kesi iliyofunguliwa na wanaharakati Counties Development Group.

Nairobi, Kenya. Mahakama Kuu imetoa amri ya kuzuia mabaraza yote ya kaunti kupitisha au kutekeleza hoja ya kuanzishwa mabaraza ya wananchi, jambo ambalo linatajwa kuwa pigo kwa muungano wa upinzani (Nasa).

Jaji Lilian Mutende alitoa amri ya muda Jumatatu hadi ilitakapokamilika kusikilizwa kesi iliyofunguliwa na wanaharakati Counties Development Group.

"Amri hii inatolewa kuwazuia walalamikiwa kuanzia wa nne hadi 50 na wanachama na wajumbe wa mabaraza ya kaunti kutoanzisha mchakato wa kuteua wajumbe, timu na waangalizi wa Baraza la Watu,” inasema amri.

Kesi iliyofunguliwa Jumatatu mchana ikiomba kuwazuia wawakilishi kutoatekeleza hoja iliyowasilishwa na kufikishwa mbele yao kwa ajili ya kuteua au kuchagua wanachama au wajumbe au waangalizi wa mabaraza ya wananchi.

Amri ya Jeji Mutende itadumua hadi Januari 28 mwaka ujao wakati usikilizwa wa kesi ukiendelea. Hata hivyo, mkuu wa sekretarieti ya Nasa walioanzisha utaratibu wa kuunda mabaraza ya wananchi, Norman Magaya alitupilia mbali amri hiyo akisema “upuuzi".