Ndugu waanza kupewa Sh1milioni ajali ya kivuko cha Mv Nyerere

Mmoja wa liopoteza ndugu katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere, Stanislaus Mpungu kutoka kijiji cha Buguza kisiwa cha Ukara akisaini nyaraka kabla ya kukabidhiwa Sh2 milioni za mkono wa pole kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kutolewa Sh1 milioni kwa kila aliyepoteza maisha katika ajali ya kivuko hicho. Mpungu amepoteza watoto wawili. Picha na Peter Saramba

Muktasari:

  • Ndugu wanaopewa fedha hizo ni waliopoteza wapendwa wao katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere pamoja na manusura 41.
  • Fedha hizo zinatolewa kufuatia agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe


Ukerewe. Watu 137 waliopoteza ndugu katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere wameanza kupokea mkono wa pole wa Sh1 milioni kwa kila marehemu aliyetambuliwa na kuchukuliwa kwa mazishi.

Awali,  ndugu hao walishakabidhiwa mkono wa pole wa Sh500, 000 kwa kila mwili uliotambuliwa.

Wameanza kupokea fedha hizo kuanzia leo asubuhi Jumanne Septemba 25, 2018.

Nyongeza ya Sh1 milioni ni agizo la Rais John Magufuli alilolitoa janam akitaka  fedha zote za rambirambi zinazochangwa na mashirika, taasisi, makampuni na watu binafsi kutumika kupewa wafiwa.

Fedha hizo pia zitatumika kujenga uzio na makaburi wanakozikwa baadhi ya waliokufa kwenye ajali hiyo iliyotokea Alhamisi Septemba 20, 2018.

Soma Zaidi: