Ngasa yamkuta Sauzi

Muktasari:

Ngassa, ambaye alijiunga na timu hiyo msimu wa 2014/15 kwa mkataba wa miaka minne, alivunjiwa mkataba wake wiki iliyopita kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Dar es Salaam. Kitendo cha mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania kuvunjiwa mkataba wake na klabu ya Free State ya Afrika Kusini, kimechukuliwa kama kujimaliza kisoka.

Ngassa, ambaye alijiunga na timu hiyo msimu wa 2014/15 kwa mkataba wa miaka minne, alivunjiwa mkataba wake wiki iliyopita kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Ofisa Maendeleo wa Shirikisho la Soka Tanzania, Jemedari Said aliliambia gazeti hili kuwa alitegemea Ngassa kutodumu Afrika Kusini.

“Nilitegemea kabisa kuwa Ngassa hatomaliza mkataba wa miaka minne, ambao alisaini kule, lakini sikutarajia kama ingekuwa mapema kiasi hiki. Haya yote yanayomkuta ni matokeo ya maisha aliyojitengenezea mwenyewe tangu siku za nyuma.