Ngeleja ataka m’kiti, mtendaji wachunguzwe

Muktasari:

  • Mwanakijiji Charles Makoye alimweleza mbunge huyo kuwa, tangu mifuko hiyo ipelekwe haijatumika na haijulikani ilipo hivyo kukwamisha ujenzi wa zahanati.

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwakamata na kuwachunguza Mtendaji wa Kijiji cha Lugongo, Shilanga Mahila na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Fikiri Kasoma kwa tuhuma za upotevu wa mifuko 48 ya saruji iliyotolewa na mfuko wa jimbo. Alitoa agizo hilo juzi katika Kijiji cha Lugongo, alipofanya ziara kuhamasisha maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.

Mwanakijiji Charles Makoye alimweleza mbunge huyo kuwa, tangu mifuko hiyo ipelekwe haijatumika na haijulikani ilipo hivyo kukwamisha ujenzi wa zahanati.

Akijibu tuhuma hizo, Kasoma alisema saruji hiyo ipo lakini imeganda kwa sababu ya kukaa muda mrefu bila kutumika. Naye Mahila alisema: “Siasa zisizo na tija, ndizo zimetufikisha hapa leo.”