Nokia yaja kivingine kuuteka ulimwengu wa ‘smartphone’

Muktasari:

Pamoja na kuzindua simu ya smartphone, pia kampuni hiyo imezindua upya simu aina ya Nokia 3310 ambayo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza miaka 17 iliyopita.

Kwa kile tunachoweza kusema ni mapinduzi makubwa  katika ulimwengu wa teknolojia, kampuni ya Nokia imezindua aina mpya ya simu za ‘smartphone.’

Pamoja na kuzindua simu ya smartphone, pia kampuni hiyo imezindua upya simu aina ya Nokia 3310 ambayo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza miaka 17 iliyopita.

Zaidi ya simu milioni 126 zilitengezwa kabla ya kuondolewa katika soko 2005.

Simu mpya iliyokarabatiwa yaani 3310 itauzwa chini ya leseni ya kampuni ya Finland ya HMD Global ambayo pia imezindua simu kadhaa za Nokia aina ya smartphone.

Mtaalam mmoja alisema ni njia nzuri ya kuzindua simu za Nokia.

''Simu hiyo ya 3310 ilikuwa ya kwanza katika soko na inasubiriwa na wengi'' ,alisema Ben Wood, mshauri wa kiteknolojia.

''Hatua hiyo ya kuzindua upya Simu ya 3310 ni wazo zuri na tunataraji itauza kwa wingi''.alisema

Simu mpya za smartphone ni  Nokia 6 na Nokia 6 Art Black. Wataalamu wa Teknolojia wa kampuni hiyo wanasema  simu zote zimeunganishwa na  Android Nougat na msaada wa Google.