Zaidi ya nyumba 50 zabomolewa Tabora

Muktasari:

  • wamiliki wa Nyumba hizo ambazo zimevunjwa imedaiwa kwamba   walivamia maeneo hayo yaliyokuwa yamepimwa tangu mwaka 1958.

Zaidi ya nyumba 50 zilizokuwa zimejengwa katika eneo la shule ya sekondari Tabora wasichana zimebomolewa kwa madai kuwa wamevamia eneo la shule.

Mkuu wa Idara ya Mipango miji mkoani Tabora, Asanga Mwakalukwa amesema ubomoaji huo umebarikiwa na vikao vyote vya Manspaa ya Tabora na kwamba wakazi hao wamevamia maeneo hayo yaliyokuwa yamepimwa tangu mwaka 1958.

“Wavamizi hao walipewa taarifa muda mrefu lakini walipuuzia hivyo tumeamua kubomoa ili kurudisha maeneo ya shule kwa ajili ya kufanyia shughuli nyingine za miradi,” amesema Mwakalukwa

Mwanasheria wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Richard Lugomela, amesema ubomoaji huo ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa la  Aprili mwaka huu wakati alipokuwa ziara ya kikazi ambapo aliagiza watu wote waliovamia maeneo ya shule kuondoka.

Lugomola amesema eneo hilo lililokuwa limevamiwa lilikuwa na visima 11 ambavyo vingewasaidia wanafunzi kupata maji kwa karibu tofauti na ilivyosasa