Ofisi ya Ridhiwani Kikwete inaungua

Jengo la ofisi ya mbunge wa chalinze Ridhiwan Kikwete ikiwa inaungua moto. Picha na Julieth Ngarabali.

Muktasari:

Kazi ya kuuzima moto inaendelea

Pwani. Ofisi ya Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete inaungua moto muda huu.

Moto ambapo chanzo chake hakijajulikana unawaka kwa kasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amesema leo Juni 17, 2018 kwamba polisi na wananchi wapo eneo la tukio wakiuzima.

Diwani wa Bwilingu ilipo ofisi hiyo, Lucas Lufunga amesema kasi ya moto huo ni kubwa na wameshatoa taarifa kwa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.

Tutaendelea kukujuza kuhusu taarifa hii.