Onyesho la Harusi kufanyika Mei 12-13

Muktasari:

  • Akizungumza na Waandishi wa habari, Meneja Biashara Hamis Omary amesema maonesho hayo ni ya kipekee kwa Afrika mashariki na pwani na hufanyika mara moja kwa kila mwaka.

Dar es Salaam. Maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanatarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip Oyststerbay Jiji Dar es salaam ili kuwapatia maharusi uwanja wa kuchagua mahitaji yao yote kwa ukamilifu siku ya harusi yao.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Meneja Biashara Hamis Omary amesema maonesho hayo ni ya kipekee kwa Afrika mashariki na pwani na hufanyika mara moja kwa kila mwaka.

"Tunawatangazia jamii kwa ujumla watarajie maonesho yakuvutia kuburudisha pamoja na nyakati rahisi kwa bwana  Harusi na bibi  harusi kuandaa vitu vyao vya harusi, vilevile kutakuwa na mitindo mipya mingi kutoka kwa wauzaji bora katika sekta ya harusi kila maonesho yanavyoendelea kukua kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine ndivyo ubora unavyoendelea kuongezeka" amesema