PAC wadai kudharauliwa

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Aesh Hilaly

Muktasari:

Wajumbe wa kamati hiyo waligoma kujadili hesabu hizo kwa maelezo kuwa, PSPF haina bodi  hivyo Katibu wa Fedha ndiye alipaswa kufika mbele ya kamati yao.

Dodoma. Katibu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amedaiwa kuidharau Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kujadili hesabu za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Wajumbe wa kamati hiyo waligoma kujadili hesabu hizo kwa maelezo kuwa, PSPF haina bodi  hivyo Katibu wa Fedha ndiye alipaswa kufika mbele ya kamati yao.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amesema PAC haitaki dharau na kuburutwa na Serikali kwani Bunge lina mamlaka.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aesh Hilaly amesema ripoti hiyo ni muhimu kutokana na kuhitajika bungeni na kwamba, kutofika kwa katibu mkuu kumewakwamisha.