Pambano la ndondi kati ya Cheka na Debeman laota mbawa

Bondia,Cosmas Cheka 

Muktasari:

Pambano hilo la raundi 10 la uzito wa kilogramu 64 limebadilisha mtizamo wa mamia ya mashabiki waliojitokeza kulishuhudia.

Dar es Salaam. Pambano la ndondi la kimataifa kati ya Mtanzania Cosmas Cheka na Jason Debeman, raia wa Afrika Kusini limeingia dosari baada ya Debeman kugoma kupanda ulingoni usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Pambano hilo la raundi 10 la uzito wa kilogramu 64 limebadilisha mtizamo wa mamia ya mashabiki waliojitokeza kulishuhudia.

"Siwezi kupigana na sitofanya hivyo.” Ilikuwa kauli ya Debeman akisisitiza kutozichapa kwenye pambano hilo akisema alisaini mkataba ili kuzichapa na Ibrahim Class na si Cheka.

Mashabiki waliojitokeza kwa wingi Diamond Jubilee sasa wanalazimika kushuhudia pambano kati ya Dulla Mbabe na raia wa China, Chengbo Zheng.