Pato halisi la Taifa limeongezeka kwa zaidi ya Sh3 trilioni

Waziri wa Fedha wa Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha bungeni taarifa ya hali ya uchumi wa taifa katika mwaka 2017 na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2018, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Waziri amesema pato la kila mwananchi limeongezeka kutoka Sh 2.1 milioni mwaka 2016 mpaka  Sh 2.3 kwa mwaka.


Dodoma. Serikali imesema Pato Halisi la Taifa limeongezeka kutoka Sh47.1 mwaka 2016 trilioni mpaka Sh50.5 trilioni mwaka jana.

Hayo yamesemwa  leo Juni 13 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akieleza mwenendo wa uchumi kwa mwaka 2017.

"Sekta zilizochangia kuimarika kwa pato hilo ni uchimbaji madini na mawe iliyokua kwa asilimia 17.5, uchukuzi na usafirishaji mizigo asilimia 16.6 na habari na mawasiliano asilimia 14.7," amesema Waziri Mpango.

Kutokana na kuimarika kwa pato la taifa, waziri alisema hata pato la mtu mmoja mmoja nalo likiimarika.

Waziri amesema pato la kila mwananchi limeongezeka kutoka Sh 2.1 milioni mwaka 2016 mpaka  Sh 2.3 kwa mwaka.