Picha ya Mtanzania anayeteswa na Mchina yampeleka Mwigulu Geita

Muktasari:

Mwigulu amesema hayo leo baada ya kuwasili mkoani Geita kwa ziara ya kikazi.

Geita. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema mfanyakazi wa mgodi wa Nyamhuna ambaye picha zake zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia baada ya kuteswa na mwajiri wake, yuko hai.

Mwigulu amesema hayo leo baada ya kuwasili mkoani Geita kwa ziara ya kikazi.

Sehemu ya mgodi huo ambao uko eneo la Katoro mkoani Geita, inamilikiwa na raia wa Kichina ambao mmoja wao anatuhumiwa kumshushia kipigo mfanyakazi huyo wa Kitanzania kwa kushirikiana na walinzi wa mgodi huo kwa madai kuwa ameuibia mgodi.

Picha za kijana huyo zimeendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha mwajiri huyo akimfanyia vitendo vya kikatili kijana huyo.

Hata hivyo, Waziri alienda hadi Gereza la Geita alikowekwa mahabusu mfanyakazi huyo ambaye mwajiri wake amemshtaki kwa kosa la wizi na kuzungumza naye.

“Nimemuona na kujiridhisha kuwa ndiye baada ya kufanya naye mahojiano na hata mavazi yake ni yale yale anayoonekana nayo kwenye picha inayosambaa mitandaoni. Pia ana makovu mengi mwilini,” amesema Mwigulu.

Habari zaidi soma Gazeti letu la Mwananchi.