Wednesday, May 16, 2018

Pinda ataja nidhamu kazini, elimu kuwa siri maendeleo ya China

 

By Kelvin Matandiko, Mwananchi kmatndiko@mwananchi.co.tz

 Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ametaja mambo manne yaliyoifanya China kuiacha Tanzania katika maendeleo, ikiwamo kujenga dhana ya maendeleo kwa watu wake kupitia kazi.

Alisema uzoefu wake kwa Taifa hilo, mambo yaliyowaletea maendeleo yanaweza kuikomboa Tanzania katika umaskini.

Pinda alisema hayo jana katika uzinduzi wa kituo cha utoaji huduma za kitaaluma cha China kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Alisema jambo la pili ni nchi hiyo kudhibiti rushwa, uadilifu wa viongozi wao, nne ni uwekezaji katika sekta ya kilimo cha mpunga na elimu.

Alisema kwamba katika sekta ya elimu, Taifa hilo liliunganisha kila mahitaji ya msingi katika jamii na mfumo wa elimu yake.

Naye Waziri wa Mambo Nje, Balozi Augustine Mahiga alisema kituo hicho kitachagiza shughuli za uchumi na kijamii nchini na kwamba, hatua hiyo imetokana na uhusiano mzuri ambao umekuwapo muda mrefu.

-->