Pogba alianzisha EPL kwa rekodi tamu

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ameweka rekodi katika Ligi Kuu ya England kwa kupachika bao la kwanza la msimu mpya wa ligi hiyo.

Pia, Man United imekuwa timu ya kwanza msimu huu kupata penalti tena ya mapema (dakika tatu) kwenye mchezo dhidi ya Leicester City kwenye dimba la Old Trafford mjini Manchester.

Beki wa Leicester City, Daniel Amartey aliunawa mpira kwenye eneo la hatari na mkwaju wa penalti wa Pogba ulimshinda kipa Kasper Schmeichel na kuipa Man United bao la kuongoza.

Katika mchezo huo wa ufunguzi, Kocha Jose Mourinho amemfanya Pogba kuwa nahodha wa Man United. Licha ya kupata bao la mapema, kwenye mchezo huo Leicester City ilionekana kuwa moto na kutengeneza nafasi za mashambulizi pamoja na kumiliki sehemu kubwa ya mchezo. Hata hivyo, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Man United ilikuwa mbele kwa bao 1-0.

VIKOSI:

MANCHESTER UNITED XI: De Gea; Darmian, Bailly, Lindelof, Shaw; Fred, Pogba (c), Pereira; Mata, Sanchez na Rashford.

Subs: Grant, Smalling, Young, Fellaini, McTominay, Martial, Lukaku

 

LEICESTER XI: Schmeichel; Amartey, Morgan (c), Maguire, Chillwell; Ndidi, Silva; Ricardo, Maddison, Gray na Iheanacho.

Subs: Ward, Evans, Fuchs, Iborra, Albrighton, Ghezzal, Vardy