Polisi Tanzania wabaini gari lililomteka Mo Dewji

Muktasari:

Leo Ijumaa Oktoba 19, 2018 Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Tanzania, Simon Sirro amesema wamebaini gari iliyotumika kumteka mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ina namba za nje ya Tanzania

Dar es Salaam. Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Tanzania, Simon Sirro amesema gari iliyotumika kumteka mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ilikuwa na namba za nje ya Tanzania.

Sirro ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 19, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kutaja namba za gari hiyo kuwa ni AGX 404 MC.

Bilionea huyo alitekwa na watu wasiojulikana Alhamisi asubuhi ya Oktoba 11 katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam alikokwenda kwa ajili ya kufanya mazoezi.

Sirro amesema baada ya uchunguzi wa kamera za CCTV wamebaini risasi iliyotumika, “Ina ukubwa wa milimita 9, CCTV zimetusaidia sana ikiwamo kulitambua gari lililotumika.”

Amesema walipofuatilia walibaini gari hilo lilikwenda maeneo ya Masaki hadi maeneo ya Kawe, sasa wanafuatilia kama walikwenda Silver Sand au wapi.

“Tumefanya kazi kubwa kuhakikisha pale ilipopotelea tunapapata,” amesema IGP Sirro.

“Uchunguzi  unaonyesha gari limetokea nchi jirani na watu wetu wamekwenda mpaka mpakani na kuona gari ya muonekano huo ilipita Septemba 1, 2018.”

Amesisitiza, “tumewasiliana na wenzetu wa Interpol ili kujua nani aliyekuwa nayo na sisi tumehakikisha watu wetu wanazunguka hizo nchi.”

“Ndugu zangu wenye uwezo wa kuwa na silaha na fedha ni ukweli ukajiokoa na silaha yako. Ni ukweli unaweza kufanyia tukio na mtu si Mtanzania. Tulikuwa tunajaribu kupitia, Mo ana silaha lakini siku hiyo hakuwa nayo, huwa anatembea na dereva lakini siku hiyo hakuwa naye,” amesema .

Amesema mtu anapotafuta fedha mara nyingi huangalia mwenye fedha.

“Ni vizuri kujilinda na niwaombe tupeane taarifa za kweli na si za majungu na kuumiza mwingine. Mtu anasema Mo yupo hapa, unakwenda, unatumia mbwa, askari, magari hukuti mtu,” amesema.

Amesema mpaka sasa wanawashikilia watu wanane kati ya 27 waliokuwa wamekamtwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Amesema katika operesheni mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya wamefanikiwa kukamata magari na silaha mbalimbali ikiwamo kumi aina ya AK 47.

Watu 104