Wednesday, July 11, 2018

Polisi ajiua kwa kujipiga risasi shingoni

 

By Anthony Mayunga, Mwananchi amayunga@mwananchi.co.tz

Serengeti. Askari wa Kituo cha Polisi Natta, Mara Nelson William, amejipiga risasi akiwa kituoni hapo na kufariki dunia leo.

Akizungumza na MCL Digital leo Julai 11, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mara, Juma Ndaki amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa askari huyo alijiua kutokana na mgogoro wa kifamilia kati yake na mkewe.

“Alijipiga risasi shingoni ambayo ilifumua kichwa chake, ilikuwa majira ya 9 alasiri akiwa kazini kwake,” amesema.

-->