Polisi wachunguzwa kwa kula chipsi bila kulipa

Muktasari:

Askari hao zaidi ya watatu wanadaiwa kuagiza watengenezewe chipsi na mayai na kukataa kulipa.

Shinyanga. Polisi Mkoa wa Shinyanga inafanya uchunguzi wa madai ya askari wake kula chipsi na kukataa kulipa kisha kuanzisha fujo baada ya kudaiwa fedha.

Askari hao zaidi ya watatu wanadaiwa kuagiza watengenezewe chipsi na mayai na kukataa kulipa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne amesema tukio hilo lilitokea Agosti 13 eneo la Mshikamano Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga saa nne usiku.