Polisi wazingira soko la Sido

Mbeya. Polisi wameimarisha ulinzi kuzunguka soko la Sido ambalo limeteketea  kwa moto kwa lengo la kuwazuia wafanyabiashara kuendelea n ujenzi wa vibanda vya kudumu.

Polisi wamezunguka eneo la soko tangu usiku wa kuamkia Leo wakiwa na silaha za moto na mabomu ya machozi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga ametoa sababu mbili za kumwaga polisi wengi eneo hilo akidai kwamba wanatekeleza agizo la Serikali  kuwazuia wafanyabiashara hao kujenga vibanda hivyo hadi watakapopata kibali .

Pia  amesema  wanazuia msongamano wa watu ndani ya soko hilo ili kutoa nafasi nzuri  kwa kamati iliyoundwa na kamati ya ulinzi na usalama ya  kuchunguza chanzo cha moto huo na hasara iliyojitokeza ili kufanya kazi hiyo kwa uhuru zaidi.