Polisi yakemea wavamizi wa migodi

File Photo

Muktasari:

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Murilo Jumanne alisema hawatawavumilia wachimbaji wa aina hiyo.

Kahama. Polisi mkoani Shinyanga imeonya wachimbaji wadogo wa madini wanaovamia maeneo yanayomilikiwa kihalali na watu wengine.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Murilo Jumanne alisema hawatawavumilia wachimbaji wa aina hiyo.

Kauli hiyo inatokana na wachimbaji wadogo wa machimbo ya almasi kwenye Mgodi wa Nyangh’wale uliopo Halmashauri ya Mji wa Kahama, kuvamia eneo la mwekezaji na kuanza kuchimba.