Polisi yapambana na majambazi Mkuranga

Muktasari:

Timu ya Mwananchi iliyo eneo la tukio imeshuhudia  magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.

Dar es Salaam. Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.

Timu ya Mwananchi iliyo eneo la tukio imeshuhudia  magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.

Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkurang, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru  zimefungwa kutokana na mapambano hayo.