Profesa Lipumba atafuta suluhu na Maalim Seif

Picha na Joyce Mmasi

Muktasari:

Lipumba amesema anaamini kuwa mazungumzo hayo yataweza kuzaa matunda na kurejesha hali ya kawaida ndani ya chama hicho.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema anawasiliana na wazee na waasisi wa chama hicho Zanzibar ili kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo baina ya viongozi wakuu wa chama hicho.

Lipumba amesema anaamini kuwa mazungumzo hayo yataweza kuzaa matunda na kurejesha hali ya kawaida ndani ya chama hicho.

Amesema yeye kama mwenyekiti wa taifa anamtambua Maalim Seif kama katibu mkuu wa chama hicho na kumtaka wakati  wowote kufika ofisini kuendelea na kazi zake za chama.