Thursday, January 12, 2017

Profesa Lipumba atema cheche Morogoro

 

By Hamida Shariff, Mwananchi hshariff@mwananchi.co.tz

Morogoro. CUF ndiyo chama cha siasa kinachoweza kupambana na mafisadi, dhuluma na uonevu na siyo vyama vingine.

Hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahimu Lipumba aliyoitoa

kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege mjini  Morogoro.

Profesa Lipumba amesema CCM na Chadema haviwezi kupambana na ufisadi kwa sababu bado vina baadhi ya viongozi waliowahi kutuhumiwa kuhusishwa na ubadhirifu.

Pia, amewataka wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea udiwani kupitia chama hicho, Abeid Mlapakolo ili alete mabadiliko ndani ya kata yao.

-->