Profesa Mkumbo aanza kazi na mradi wa mabilioni

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (kulia)

akisaini mkopo wa Sh600 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tabora. Picha ya mtandao

Muktasari:

  • Profesa Mkumbo alisaini mkopo  huo juzi, mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya  utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo. Mkopo umetolewa na Benki ya Exim ya India.
  • Awamu ya pili ni ujenzi wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza itaanzia Kijiji cha Solwa (kilichopo Wilaya ya Shinyanga Vijijini) hadi Mji wa Nzega, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd ya India.

Tabora. Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, ameanza kazi kwa kusaini mkopo wa Sh600 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tabora.

Profesa Mkumbo alisaini mkopo  huo juzi, mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya  utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo. Mkopo umetolewa na Benki ya Exim ya India.

Awamu ya pili ni ujenzi wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza itaanzia Kijiji cha Solwa (kilichopo Wilaya ya Shinyanga Vijijini) hadi Mji wa Nzega, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd ya India.

Sehemu ya Pili inaanzia Mjini Nzega mjini hadi Manispaa ya Tabora kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, ujenzi utafanywa na Kampuni ya L&T ikishirikiana na kampuni ya Shriram zote kutoka India.