RC ‘awatishia nyau’ madiwani

Muktasari:

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga wakati akitoa maelekezo kwa baadhi ya madiwani wa halmashauri za wilaya ya Uvinza na Buhigwe.

Kigoma. Watumishi wa umma, viongozi wa siasa na wananchi watakaobainika kukata miti na kuharibu misitu mkoani hapa, wataadhibiwa bila kujali wadhifa na majukumu yao kwa jamii.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga wakati akitoa maelekezo kwa baadhi ya madiwani wa halmashauri za wilaya ya Uvinza na Buhigwe.

“Wapo pia baadhi ya madiwani wanaoharibu mazingira kwa kukata miti kiholela, hawana vibali vinavyoruhusu kufanya hivyo. Tukikukamata hatutajali udiwani wako, tutakuburuta mahakamani ukajibu tuhuma zako,” alisema Maganga.

Diwani wa viti maalumu kutoka Uvinza, Salome Luhingulanya alisema madiwani wana dhamana ya kuhakikisha wananchi wanatii na kufuata sheria za nchi.