Rahco: Tutaendelea kuvunja nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya reli

Muktasari:

Kadhalika imesema   inakusudia kuvunja nyumba nyingine kadhaa zilizojengwa katika korido inapotakiwa kupita reli kutoka Dar hadi Bagamoyo.


Dar es Salaam. Kampuni hodhi ya rasilimali za reli (Rahco)imesema mpaka sasa nyumba 485 zimevunjwa  kutokana na kujengwa kwenye hifadhi ya reli.

Kadhalika imesema   inakusudia kuvunja nyumba nyingine kadhaa zilizojengwa katika korido inapotakiwa kupita reli kutoka Dar hadi Bagamoyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Rahco na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)Masanja Kadogosa alisema watu hao wengi wanajijua ni wavamizi wa eneo hilo  kwani wapo waliokwenda mipango Miji ili kupewa hati ya kumiliki kiwanja na  wakajulishwa ni mali ya reli.

"Walijulishwa lakini bado wakaamua kuwa wakaidi wamejenga nyumba za kifahari ikiwamo ghorofa, tutawapa taarifa rasmi navunja nyumba hizo bila kuwalipa fidia yoyote," alisema Kadogosa.