Raia wawili wa China matatani kwa kumteka nyara mwenzao

Muktasari:

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro alisema jana kwamba mfanyakazi aliyetekwa nyara alikutwa kwenye hoteli ya Palm Beach akiwa hajitambui na alikuwa na majeraha usoni.

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imewakamata raia wawili wenye asili ya China wakituhumiwa kumteka nyara mfanyakazi wa Le Grade Cassino, Liu Hong (48) wakitaka walipwe fedha.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro alisema jana kwamba mfanyakazi aliyetekwa nyara alikutwa kwenye hoteli ya Palm Beach akiwa hajitambui na alikuwa na majeraha usoni.

Sirro alisema Mchina huyo alitekwa Oktoba 23, saa kumi na moja alfajiri na watu wasiofahamika. Alisema Polisi ilipopata taarifa ilituma kikosi kazi cha kupambana na wizi wa makosa ya kimtandao ambacho kilibaini kuwa watekaji nyara hao walikuwa kwenye hoteli hiyo.