Rais Erdogan atua na wafanyabiashara 85

Rais wa Uturuki, Recep Erdogan

Muktasari:

Baada ya kuwasili, Rais Erdogan ambaye pia ameambatana na mke wake, Emine Erdogan aliepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Dar es Salaam. Rais wa Uturuki, Recep Erdogan amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, akiwa ameambatana na wafanyabiashara 85 wa nchi hiyo.

Baada ya kuwasili, Rais Erdogan ambaye pia ameambatana na mke wake, Emine Erdogan aliepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Pia, Rais Erdogan ameambatana na mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje, Mevlüt Çavuşoğlu; Waziri wa Uchumi, Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Berat Albayrak.