Rais Lula da Silva wa Brazil kushtakiwa

Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva.

Muktasari:

Kiongozi huyo wa zamani ambaye ni mshauri wa rais wa sasa, Dilma Rousseff anadaiwa kuyumbisha uchunguzi wa ufisadi katika kampuni taifa ya mafuta ya Petrobras.

Brasilia, Brazil. Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, ameshtakiwa kwa madai ya kujaribu kuzuia uchunguzi wa ubadhirifu katika kampuni ya taifa ya mafuta ya Petrobras. Kiongozi huyo wa zamani ambaye ni mshauri wa rais wa sasa, Dilma Rousseff anadaiwa kuyumbisha uchunguzi wa ufisadi katika kampuni hiyo. Silva amekuwa chini ya uchunguzi wa madai mbalimbali.

Mamia ya wanasiasa, wakurugenzi pamoja na watu wengine mashuhuri wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi wa kampuni ya Taifa ya mafuta nchini humo.(DW)