Rais Mafuguli, haya ndio matarajio!

Rais John Magufuli

Muktasari:

Kikao hicho jana kilipitisha jina la Rais Magufuli kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika uchaguzi utakaofanyika leo, kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho, Christopher ole Sendeka.

Dar/ Mikoani. Siku moja kabla ya Rais John Magufuli kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, wenyeviti na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wamemtaka kufanya mabadiliko makubwa ya kukisaficha chama.

Kikao hicho jana kilipitisha jina la Rais Magufuli kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika uchaguzi utakaofanyika leo, kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho, Christopher ole Sendeka.

Makada walioulizwa na Mwananchi swali la ‘Wanataka Magufuli aifanyie nini CCM’, wengi wamemtaka aondoe makundi yaliyopo kwenye chama, huku baadhi wakitaka akisafishe kwa kushughulikia mafisadi na watendaji wasio waaminifu.