Rais Magufuli atengua uteuzi wa mkurugenzi Butiama

Muktasari:

Ni kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yake

Dar es Salaam.  Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Butiama mkoa wa Mara, Solomoni Ngilule kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yake.

Uamuzi huo umetangazwa leo Jumanne Januari 23 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo wakati akizungumza na wanahabari.

Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe amesema, “Rais Magufuli ambaye ana dhamana na wizara hii amechukua jukumu hilo kutokana na kilichojiri katika halmashauri hiyo,” amesema na kuongeza.

“Pia ametoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Tamisemi kuchukua hatua kwa mweka hazina wa halmashauri ya Butiama ambaye alikuwapo wakati ubadhirifu wa fedha unatokea.”